Wakati wa Ibada ya Wafu ya moyo wa marehemu Kardinali wa Ujerumani Joachim Meisner (+83), mridhi wake, Kardinali wa Cologne Woelki, alisema kuwa Meisner alifariki kati ya Saa kumi na mbili na saa moja alfajiri alipokuwa likizoni katika maeneo ya Bad Füssing (Bavaria). Takriban saa kumi na mbili alfajiri, kelele kutoka kwenye chumba cha Meisner zilisikika. Kati ya saa kumi na moja na saamoja alfajiri, rafikiye alienda kwenye chumba chake kwani walikuwa wakimsubuiri kwenye Sakristi, lakini hakukuwa na jibu lolote. Meisner alipatikana kitini akiwa ameketi huku akikumbatia kijitabu cha maombi, na akikwa amekodoa macho yake.